Tuesday 8 December 2015



IMG_6094
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akiongozana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara tu baada ya kumpokea alipowasili ofisini kwake akiwa ameongozana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (hawapo pichani).
Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameelezea kufurahishwa kwake na uwapo wa mradi wa kusaidia vijana wa kitanzania kujifunza ujasirimali na kujitegemea.
Akizungumza katika shughuli za uzalishaji mali za vijana wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma alisema kwamba shughuli wanazofanya vijana hao zinamsisimua sana.
 “Tunafurahi sana mimi na  wenzangu kutembelea mradi huu unaofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao unachochea ujasirimali miongoni mwa vijana. Sote tunajua kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanaume kwa wanawake wameelimika lakini hawana ajira rasmi. Na suala la ujasiriamali ni kitu ambachio mtu anaweza kujifunza, na ujasiriamali unatoa fursa  kwa vijana kujiunga katika kundi la wafanyakazi kwa kujiajiri wenyewe.
“Tunajua kwamba kupitia shughuli zinazofadhiliwa na ILO katika ngazi ya jamii na kwa kufuata maelekezo ya serikalai za mtaa vijana wanaanzisha biashara mbalimbali binafsi au na jamii. Kiwanda cha kutengeneza sabuni ni mfano mzuri sana. Tunaona kwamba mradi huu unawaongezea kipato na hivyo kuweza kusaidia familia zao na kupeleka watoto shuleni na kuboresha lishe . Kwa ufupi mradi kama huu unasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili kaya maskini Kigoma” alisema Rodriguez
ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na  kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
IMG_6098
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya (kushoto) akibadilishana 'Business card' na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.
Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.
Aidha alisisitiza haja ya jumuiya ya kimataifa kuusaidia mkoa Kigoma katika nyanja mbalimbali za kiuchumi hasa katika eneo la ajira kwa vijana kutokana na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo katika kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi kutoka nchi za maziwa makuu kwa upendo.
Rodriguez alisema pamoja na ombi hilo Mratibu huyo wa shughuli za kimataifa ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) alisema wao kama UN wakifanyakazi pamoja wataendelea kutoa misaada kwa wakimbizi hasa uanzishaji wa miradi ya kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Idadi ya watu (UNPFA), Dkt. Natalia Kanem alisema kuwa kupatiwa mitaji na kuanzisha vikundi vya uzalishaji kwa vijana na wanawake kunasaidia kuongeza ajira lakini pia kusaidia kupunguza ongezeko kubwa la idadi ya watu bila mpangilio.
Katika risala yao kwa uongozi huo wa Umoja wa Mataifa vijana kutoka Nyakitonto Youth Development  Tanzania wamesema kuwa misaada iliyotolewa kwao imewasaidia kupata ujuzi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ikiwa ni sehemu ya kujiajiri na kujiongezea kipato ili waweze kuendesha maisha yao bila utegemezi.
IMG_6105
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akitoa taarifa ya mkoa wake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe ofisini kwa Mkuu huyo wa mkoa.
Hata hivyo vijana hao katika risala yao iliyosomwa na Meneja miradi wa shirika hilo, Anjelina Gulanywa walisema kuwa pamoja na mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto utaalam mdogo, mitaji na vitendea kazi vya kisasa ili kufanya shughuli zao kuwa na mafanikio zaidi.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu,  Issa Machibya alieleza kuridhishwa kwake na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kusaidia miradi mbalimbali mikoani mwake ambayo inasadia wananchi kukabiliana na umaskini.
Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR),Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Idadi ya watu (UNFPA) ,Shirika la kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia watoto( UNICEF), Shirika la Kuhudumia wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
IMG_6134
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake katika mkoa wa Kigoma kwa Mkuu wa mkoa huo, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6123
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) nchini, Magnus Minja akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na  kuhudumai familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao unaofadhiliwa na shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6147
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasilisha Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Golas-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
IMG_6152
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya Khanga ya 'miaka 60 ya UNFPA Tanzania',  kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanal Mstaafu, Issa Machibya, huku Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akishuhudia tukio hilo.
IMG_6156
Malengo ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Kigoma. Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya na baadhi ya wakurugenzi katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_6161
IMG_6172
IMG_6164
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi Nyarugusu.
KUELEKEA KWENYE UKAGUZI WA MRADI WA VIJANA UNAORATIBIWA NA ILO........