Saturday 31 October 2015

User comments
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili  mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani  na kijiji hicho.
Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
User comments
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema wazo la kuanzishwa kwa  kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
 “Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na  bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
User comments
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
 “Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia  ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.
Kijiji cha Kisangara  ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
1 (11)
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi  na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
User comments
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
20151023_122610
User comments
Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.