Saturday 26 September 2015

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Tigo kwa
kushirikiana na taasisi ya Reach for Change zimezindua shindano la
wajasiriamali jamii liitwalo “Tigo Digital Change-makers”lenye lengo la kuibua mawazo ya kibunifu ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayo wakabili watotona vijana nchini.

Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez leo ametangaza uzinduzi wa shindano hilo katika mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa watu
kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu dola za kimarekani
20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya
kibunifu.

“Tigo ikishrikianana
Reach for change itatoa tuzo ya dola za kimarekani20,000 kwa kila mmoja kwa washindi
wawili ambao wataku wa na mawazo ya bunifu zaidi kiteknolojia na kidijitali yaliyo
na uwezo wa kuchangia kuleta maisha bora kwa watoto katika jamii ya kitanzania,”
alisema Gutierrez.

Aliongezeakwamba,
“Lengo letu ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidijitali ambayo yataleta na kutatua
matatizo ya nayo wakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku tukiendelea kuwekeza katika
kukuza na kuimarisha huduma zetu za mawasiliano katika maeneo yote nchini.”

Mawazo yatakayo
wasilishwa kupitia shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidijititekinolojia
ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi wa utekelezaji wa mradi husika.
Watakaopenda
kushiriki shindano hili wanaweza kutuma maombi kupitia mtandao wa
www.tigo.co.tz/digitalchangemakers, kwa 
mujibu wa Gutierrez.

Kwa upande
wake, Meneja wa nchi wa Reach for Change, Peter Nyanda, alisema licha ya kupatakitita
cha dola 20,000 washindipia watapewa vifaa vya kuendeleza utekelezaji wa mawazo
yao ikiwa ni pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wafanyakazi waandamizi kutoka Tigo
na Reach for Change.

Aidha wata unganishwa
na wajasiriamali wengine ambao tayari wamenufaika kutokana na mpangohuo.

Mchakato huu
wa kuwapata wajasiriamali jamii wakidigitali unaendana na mkakati waTigo wa kuendeleza
maisha ya kidijitalinchini.

Huu ni mwaka
wa nne mfululizo ambapo taasisizaTigo na Reach for Change zimekuwazikishirikiana
kuwasaidia wajasiriamali nchini. Jumla ya wajasiriamali watano wa menufaika na mpango
katika kipindi hiki ambao kwapamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia
jumla ya watoto zaidi ya 10,000 nchini.