Sunday 27 September 2015


HABARI YA AFYA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPHaitdjZ6qdAFEHDXoYQICqKbH4nSRxEuvfEbN9mz38jCTqJl6W3YImbQOuwzu13UNaGkr1sOOWx-rRJRrxhK4mfcS9bZ9R0dZ24hgSsdhrG8A9bCy-ErAc2EV8wzZ-bBCDi6F4kSMFDg/s1600/Dr++Revathi.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPHaitdjZ6qdAFEHDXoYQICqKbH4nSRxEuvfEbN9mz38jCTqJl6W3YImbQOuwzu13UNaGkr1sOOWx-rRJRrxhK4mfcS9bZ9R0dZ24hgSsdhrG8A9bCy-ErAc2EV8wzZ-bBCDi6F4kSMFDg/s640/Dr++Revathi.jpg
" width="640" />









Na Mwandishi Wetu, 



Ibrahim
 (jina limebadilishwa) alizaliwa nchini Tanzania na alipokuwa na umri wa
 miezi 9 tu alionekana anang’aa na hakuwa na uwezo wa kula na kukua 
vizuri kama watoto wengine wa umri wake. Alikuwa na maambukizi ya mara 
kwa mara na vipimo vya damu vilionyesha upungufu mkubwa wa damu na 
kiwango cha ukosefu wa damu kwa gm 3.5! Ibrahim alikuwa akiishi na chini
 ya robo ya kiwango cha oksijeni kinachohitajika kwenye damu na 
alihitaji haraka kuongezewa damu ili kuokoa maisha yake. Vipimo vya damu
 yake na ya wazazi wake vilithibitisha kuwa alikuwa na thalasemia kuu.





Thalassaemia
 kuu ni hali ya kurithi ambapo huwa na ukosefu wa chembe nyekundu za 
damu. Katika mwili seli shina Uboho huzalisha aina tatu za seli za damu 
katika mwili- nyekundu, nyeupe na chembe chembe za damu. Thalasemia ni 
hali ya kurithi inayoathiri seli nyekundu za damu. Hutokea wakati mtu 
anashindwa kuzalisha kiasi cha damu kinachotakiwa. Mwili wako hautafanya
 kazi vizuri kama chembechembe nyekundu za damu hazizalishi damu ya 
kutosha yenye afya.





Dkt.
 Revathi Raj wa  Hospitali za Apollo Chennai anaeleza zaidi kwamba 
thalasemia ni ya kurithi. Ni kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto kwa 
njia ya jeni. Watu ambao hurithi jeni za damu mbaya kutoka kwa mzazi 
mmoja lakini jeni za kawaida kwa mzazi mwingine wanaitwa kitaalamu 
‘career’. ‘Carriers’ mara nyingi hawana dalili za ugonjwa mwingine zaidi
 ya kuoneshwa upungufu mkubwa wa damu. Hata hivyo, wanaweza kurithisha 
jeni mbaya kwa watoto wao. Watu ambao wana wastani wa kati wa thalasemia
 wamerithi jeni mbaya kutoka kwa wazazi wote wawili. Kama ‘carriers’ 
wawili wakizaa mtoto, kuna 25% ya nafasi ya kuwa na mtoto aliyethirika.


Kwa
 mujibu wa Dkt Revathi Raj madhara ya kuacha thalassaemia bila kutibiwa 
ni pamoja na kushindwa kwa wengu, ini na moyo. Pia, inaweza kusababisha 
mifupa myembamba na migumu na mikunjo usoni. Ni kawaida kwamba watoto 
wasiotibiwa hudumaa ukuaji wa mwili na akili. Watoto wenye Thalasemia 
huwa wanakufa kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi na maambukizi 
ikiwa hali hiyo haitatibiwa.


Matibabu
 pamoja na kuongezewa damu mara kwa mara na dawa za kuzuia maambukizi 
huweza kupunguza kasi ya ugonjwa. Watoto wenye thalasemia wanaweza 
kutibiwa kwa kuongezewa damu mara kwa mara. Zoezi hili linatakiwa 
kufanyika kila baada ya wiki 3 au 4 na husaidia kuweka kiwango cha damu 
kawaida. Wakati viwango vya damu vikiwa kawaida mtu anaweza kujaribu 
kuzuia baadhi ya matatizo ya ugonjwa kwa hiyo kuzuia moyo kushindwa 
kufanya kazi na ulemavu wa mfupa na hivyo kupelekea ukuaji mzuri na afya
 kwa ujumla.


Hali
 ya Ibrahim ina maana kwamba wazazi wake walihitaji kusafiri pamoja naye
 kwa zaidi ya km 1,000 kila mwezi kwa ajili ya kuongezewa damu kutokana 
na ukosefu wa vifaa vya kutosha Tanzania. Huku kuongezwa damu 
kulihitajika ili kuendelea kwa maisha yote ya Ibrahim hii ikiwa ni hali 
ya kudumu.





Wangewezaje
 kutoa damu kila mwezi? Kwa nini hakuna mtu aliyegundua kwamba walibeba 
jeni mbovu ambazo zinaweza kuleta madhara kwa mtoto wao? Haya ni baadhi 
tu ya maswali kadhaa ambayo wazazi wa mtoto huyu wanakabiliwa nayo.








Changamoto
 nyingine iliyowakumba wazazi Ibrahim ililikuwa kwamba pamoja na kila 
kuongezewa damu kuna hatari ya madini chuma katika kila kiasi cha damu 
kinachoongezwa. Kujijenga kwa madini chuma husababisha uharibifu wa moyo
 na ini na viungo vingine. Kuepuka, kuzuia au kuchelewesha madini chuma 
kujijenga mtu anahitaji tiba ya madawa kila siku. Kwa bahati mbaya hata 
hivyo, kwa Tanzania tiba hii si rahisi hivyo kupatikana. Maisha kwa 
Ibrahim yalionekana hatarini sana mpaka baada ya familia kusikia kuhusu 
BMT kusaidia kumtibu mtoto wao mdogo na kusafiri hadi Hospitali ya 
Apollo, Chennai nchini India ambako walikutana na Dkt Revathi Raj. 
Hospitali ya Apollo, India ni jina la kuaminiwa katika BMT kwa ajili ya 
wagonjwa wa kimataifa, kama hospitali ina si tu yenye timu ya BMT 
inayosifika, lakini pia masharti magumu sana kudhibiti maambukizi ambayo
 ni muhimu kwa ajili ya wagonjwa wa BMT.


Kwa
 BMT ‘Haematopoietic’ seli shina inapatikana kutoka kwa ndugu ambaye 
hajaathirika anayeendana au mfadhili yeyote na kupandikizwa kwa mtu 
mwenye thalasemia. Kwa bahati mbaya, Ibrahim hakuwa akiendana na 
wafadhili wa familia. Hata hivyo, mfadhili waliyeendana kikamilifu 
katika shina kiini la uboho aliyejisajili nchini India aitwaye DATRI 
alitoa mwanga mpya wa matumaini.


Mkakati
 wa kupandikiza uboho kwa watoto katika Hospitali ya Apollo nchini India
 ina timu ya wataalam wenye ujuzi wa juu na mratibu wa BMT anayefanya 
kazi kama sehemu ya timu ya wataalam mbalimbali kutoa huduma 
iliyoboreshwa kwa ajili ya watoto ambao wanapata tiba ya shina. 
Hospitali za Apollo nchini India zina uzoefu mkubwa nchini humo katika 
kuhudumia watoto wachanga na wadogo wanaoendelea na upandikizaji wa seli
 za shina.





BMT
 ni tiba yenye hatari kubwa ambayo inawezekana kwa asilimia ndogo sana 
ya wagonjwa iwapo mfadhili uboho anayefaa yupo. Hata kama kiwango cha 
mafanikio ya BMT ni sawa na 95%, ni kazi ya hatari na huweza kusababisha
 kifo. Kiwango cha mafanikio hutegemea zaidi iwapo au hakuna uharibifu 
mkubwa uliofanyika kwa kiungo chochote kama vile madini chuma kwenda 
mahali pasipofaa.





Dawa
 mpya katika soko na muendelezo wa ugunduzi katika taaluma ya utabibu 
imewezesha mchakato wa upandikizaji kuwa salama zaidi, hata kwa watoto 
wachanga na watoto wadogo. Hospitali Maalum ya Apollo, imelifanya 
upandikizaji wa seli shina kwa zaidi ya wagonjwa 800 ikiwa zaidi ya robo
 kati yao waliokuwa na thalasemia na zaidi ya kufanikiwa kwa Zaidi ya 
90%.





Ujumbe
 muhimu zaidi mtu anahitajika kuchukua katika hili ni umuhimu wa kupima 
wajawazito. Vipimo vya damu vinaweza kuonyesha kama mtu ana thalasemia 
au ni ‘carrier’ kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Dkt Revathi Raj 
katika Hospitali ya Apollo Chennai anashauri kuwa ni bora kumweleza 
daktari wako kumpima mtoto wako kiwango cha ‘ferritin’ cha mtoto wako 
kama ana upungufu wa damu kabla ya maagizo ya vitamini yoyote. Ni jambo 
la kawaida kwa madaktari kutoa maelekezo ya vitamini kwa watoto ambazo 
huonyesha dalili za upungufu wa madini chuma. Hata hivyo, ni muhimu 
kuchunguza tahadhari, kwa maagizo ya kuongeza madini chuma kwa ajili ya 
upungufu wa madini hayo anemia inaweza kuwa sahihi, inaweza kusababisha 
kuzidi kwa madini chuma kwa watoto wenye aina yoyote ya thalasemia. 
Jaribio rahisi kuamua kiwango cha madini chuma, au kiwango cha 
‘ferritin’, katika mwili wa mtu linaweza kufanywa. Kama mtu anaonekana 
kuwa na upungufu wa madini chuma, lakini kiwango cha ‘ferritin’ kipo 
kawaida, pengine wana aina ya kwanza ya ‘beta thalasemia’.





Ndugu
 kuoana mara kwa mara pia husababisha mtu kuwa ‘carrier’ wa thalasemia. 
Ndoa kati ya ndugu ziepukwe kwa kuwa kuna ongezeko la ugonjwa wa kurithi
 na kama inaepukika uchunguzi wa damu kwa wanandoa kabla ya ndoa 
unashauriwa.





Tunahitaji
 pia kuongeza uelewa miongoni mwetu Watanzania juu ya umuhimu wa 
kujitolea kwa kuchangia damu na seli za shina kama msaada kuokoa maisha 
haya. Kuna matumaini kwa watoto wote kupata nafasi ya tiba kwa kuwa kuna
 wengi waliojisajili – hasa watu wazima ili kusaidia wagonjwa wote wa 
thalasemia kuu.








Imechangiwa na:




Dkt. Revathi Raj

Mtaalamu wa magonjwa ya watoto ‘Hematology’, Kupandikiza uboho (BMT)
Apollo Hospitals Chennai