Wednesday 26 August 2015

MSAADA TUTANI, HABARI YA AFYA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-Rrj1RWMpZHMvEn3HBb2cBUd8bHRVvJ_h2xdG4GibCsAfDTNvLskE7tb4cAlAy7W1yRQbitUi9jjkETEMl7ksg2Vn7useC4JX9Zyzo3frY1L0fnbEJUbvjbGK1SsUMJI1yD3dS4ls3hst/s1600/F+1.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-Rrj1RWMpZHMvEn3HBb2cBUd8bHRVvJ_h2xdG4GibCsAfDTNvLskE7tb4cAlAy7W1yRQbitUi9jjkETEMl7ksg2Vn7useC4JX9Zyzo3frY1L0fnbEJUbvjbGK1SsUMJI1yD3dS4ls3hst/s640/F+1.jpg
" width="640" />




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxGcgAZ0HBplqdar9_hyL1RZ5fUyflB1XRC-FOmH8rszu57bOP35eIt22hE5l30r1EHosSIfF4k-IO_JxSVFGCd0pG5QJV_SVbrN4MprBzk7saM7wJwMDS815HP1ATzqSyT5uP8jpS-e0U/s1600/F+2.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxGcgAZ0HBplqdar9_hyL1RZ5fUyflB1XRC-FOmH8rszu57bOP35eIt22hE5l30r1EHosSIfF4k-IO_JxSVFGCd0pG5QJV_SVbrN4MprBzk7saM7wJwMDS815HP1ATzqSyT5uP8jpS-e0U/s1600/F+2.jpg" />




Na Mwandishi Wetu ,

Kutokea
 kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani
 kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na 
maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8 
kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu
 hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa 
takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani
 Afrika inaweza kuwa wengi sana.


Watoto
 wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. 
baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, 
mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, 
kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto 
kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. Wakati 
mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa 
watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza 
kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida 
zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha
 ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo 
wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa 
mizunguko upumuaji.





Watoto,
 hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya 
umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji
 moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto 
anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake 
unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji
 kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa 
ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni 
mgumu zaidi.


Kutokana
 na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, 
Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya 
Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona 
kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na 
mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu
 miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, 
kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze 
kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa 
upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji 
unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika 
hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.


Wakati
 mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza 
hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG 
ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG) 
mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa
 ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu 
yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, 
takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia 
katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.





Uboreshaji
 wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto. 
Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande 
tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango 
bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo
 matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.





Kuna
 tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na 
mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na 
kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii 
inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya 
moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa 
vinavyowezesha  kuipata  mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na 
valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii  mtoto hapati maumivu ya 
kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji  mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto 
kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona
 kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.


Namna 
 nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali 
mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani 
(upasuaji). Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri
 wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa 
hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata 
mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.


Watu
 kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika 
kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa 
watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti 
maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya
 kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu 
zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.





Kwa
 mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo, 
Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza 
kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) 
kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika 
kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama. Daktari bingwa wa 
Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya 
ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi 
sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika 
katika moyo.





Njia
 nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa 
kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na 
kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na 
kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya 
kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa 
matibabu ya maambukizi katika  koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.





Timu
 ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai
 inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto 
duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya
 sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii 
Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro 
na magonjwa ya moyo.


Baada
 ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji 
ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji 
hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na
 maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya 
kwa muda mrefu maishani bila matatizo.





Inachangiwa na:




Dk Neville A.G Solomon

Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto

Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.