Tuesday 3 March 2015

RAIS DK. SHEIN AWAONGOZA WAUMINI WA KATIKA HITMA YA MAREHEMU SALMIN AWADH

Mar 2, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuikana Viongozi na waislamu katika kisomo cha Hitima ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishiwa Jimbo la Magomeni (CCM) iliyosomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal, Mwembeshauri Mjini Unguja. Hitma hiyo ilihudhuriwa na Waumini na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi. (PICHA ZOTE NA IKULUR)
Baadhi ya Waislamu, viongozi mbalimbali na wananchi, wakiwa katika kisomo cha Hitima ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni. Hitima hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri. 
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akitoa mawaidha baada ya kisomo cha Hitima ya Marehemu Salmin Awadh, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni. Hitima hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa shukurani kwa Viongozi mbalimbali, Waislamu na Wananchi na wapenzi wa CCM baada ya kisomo cha Hitima Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja iliyosomwa leo katika Msikiti wa Mushawal Mwembesahauri. Marehemu alifariki hivi karibuni na kuzikwa Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.