Wednesday 19 February 2014

Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye  alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo  aliouelekeza kwa mzazi huyo.  Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
nasi tutafikisha ubani wako. 
Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii 
ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDVGjsa1vKrJgwA_418jCWvOF8-8Xdk_FBPoRCtLRXd2iN0MvSU-_KDA7-KkZQcRISm72P2hS2shU9hHVX1_DfOepucumswrg-ZXpmtd_uF3kMMSWfJUW0Zs8GPhhzg9NgS6eYDRlxlq30/s1600/DSC00124.JPG" imageanchor="1" style="color: #3366cc; margin-left: 1em; margin-right: 1em; text-decoration: none;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDVGjsa1vKrJgwA_418jCWvOF8-8Xdk_FBPoRCtLRXd2iN0MvSU-_KDA7-KkZQcRISm72P2hS2shU9hHVX1_DfOepucumswrg-ZXpmtd_uF3kMMSWfJUW0Zs8GPhhzg9NgS6eYDRlxlq30/s640/DSC00124.JPG
" height="480" style="border: 1px solid rgb(238, 238, 238); padding: 2px;" width="640" />
Aida Nakawala 25
mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni
alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa
kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika
Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira
ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya
Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya
Wengi.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0p7Hl5us9ChAXWZZvbipwzAP0fMj7TYvNaQI9Gk4PNVkf6cnUHAmWP08-EPA7H-pHu1hF7-33RrB9CHqJCDEVMVOlRtSVkSOeWlmVRnKhiec8J6QOoYYtGW2QiRK8PwtpyfqlwKoyRAAO/s1600/DSC00144.JPG" imageanchor="1" style="color: #3366cc; margin-left: auto; margin-right: auto; text-decoration: none;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0p7Hl5us9ChAXWZZvbipwzAP0fMj7TYvNaQI9Gk4PNVkf6cnUHAmWP08-EPA7H-pHu1hF7-33RrB9CHqJCDEVMVOlRtSVkSOeWlmVRnKhiec8J6QOoYYtGW2QiRK8PwtpyfqlwKoyRAAO/s640/DSC00144.JPG
" height="480" style="border: medium none; padding: 0px;" width="640" />
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwN854inrGQQiK_dFKAK1PEHLAZ4eBEZbfNvfouXQKlY1kFB0WC5PROZHwKbAr1wyriXfYxc-EqK5b-HQHPCf94HynZjJf3OV7CvfT2rnI4IDsaa1GG4v64TbkjR8_cP4F9tK-CnAN4HCc/s1600/IMG_2580.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwN854inrGQQiK_dFKAK1PEHLAZ4eBEZbfNvfouXQKlY1kFB0WC5PROZHwKbAr1wyriXfYxc-EqK5b-HQHPCf94HynZjJf3OV7CvfT2rnI4IDsaa1GG4v64TbkjR8_cP4F9tK-CnAN4HCc/s1600/IMG_2580.jpg
" height="480" width="640" />
 Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8N8XPMIEJLWcobFVYLr2LjmCf0_Sk_G4Bw-PWRqu5kt3czTj_fep9U9CuGgaRwpWowsTpUAG2_Ldci9LYPGK5a1j0YORfBCatyZHG04AALRcan86dXxDTMdUBgWR3fwQ29J3OwVA3LcqS/s1600/IMG_2582.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8N8XPMIEJLWcobFVYLr2LjmCf0_Sk_G4Bw-PWRqu5kt3czTj_fep9U9CuGgaRwpWowsTpUAG2_Ldci9LYPGK5a1j0YORfBCatyZHG04AALRcan86dXxDTMdUBgWR3fwQ29J3OwVA3LcqS/s1600/IMG_2582.jpg
" height="480" width="640" />