Saturday 6 October 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba la Rideau Hall jijini Ottawa katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Canada huku akishuhudiwa na Gavana Jenerali wa nchi hiyo Mhe David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson Alhamisi Oktoba 4, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa  mara baada ya kuweka  shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4, 2012. Mbele yake ni baadhi ya veterani wa kijeshi waliohudhuria hafla hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuweka  shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar (Zanzibar chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada  ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada  Alhamisi Oktoba 4, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika ofisi ya Spika wa Bunge la Wawakilishi la Canada (House of Commons)  Mhe Andrew Sheer. Spika huyu, mwenye umri wa miaka 32, ndiye kiongozi kijana kuliko wote katika historia ya nchi hiyo waliopata kuchaguliwa kuongoza bunge hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada  ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada  Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa  nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakiongea na wanahabari katika jengo la Bunge la Seneti la nchi h
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Watanzania Richard Katambi Masalu na mkewe Patricia katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa kabla ya kuondoka kuelekea Edmonton
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa pili mbele kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Alex Massinda (mbele kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni ya Canada baada ya mazungumzo katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Canada, na baadaye kupiga nao picha ya pamoja
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Gavana Jenerali wa Canada Mhe David Johnson baada ya kuihitimisha ziara yake ya siku mbili jijini Ottawa. Baada ya hapo alielekea jijini Edmonton ambako pamoja na shughuli mbalimbali alitarajiwa kufungua mkutano wa Diaspora wa Watanzania wanaoishi Canada pamoja na wawamkilishi wa makampuni na mashirika waliotoka Tanzania kuhuduria mkutano huo.Picha na IKULU