Monday 8 October 2012

Ethiopian | 787 - Africa's First Dreamliner

Ethiopian | 787 - Africa's First Dreamliner





Default 

Sumaye amgwaya Lowassa

• Akana kuwa na uhasama naye, adai hamwogopi mtu

na Edson Kamukara
WAZIRI Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ametoa dukuduku lake la moyoni akisema hana uhasama na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na kubainisha kuwa rushwa ya kimtandao iliyokighubika Chama cha Mapinduzi (CCM), ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang’.
Sumaye ambaye amepigwa mweleka kwenye uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia wilayani Hanang’ na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu, alikutana na wanahabari kuelezea mwendo mzima wa uchaguzi huo na hatima ya CCM.
Akizungumza kwa kujiamini huku akinukuu kauli zake za nyuma kuhusu mwenendo wa rushwa ndani ya chama chake, alisema uchaguzi wa Hanang’ ulighubikwa na matumizi makubwa ya rushwa, vitisho vingi, uharamia wa kuhamisha wapiga kura usiku na maovu mengineyo mengi.
“La msingi ni kuwa mimi sijakata na wala sitakata rufaa ya kupinga matokeo wala kupeleka malalamiko katika chama changu kwa sababu yaliyokuwa yakitendeka yalikuwa yanafahamika,” alisema.
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama kuondoa uvumi uliokuwepo kuwa Sumaye na Lowassa wana ugomvi wa kisiasa hasa wakati huu wa kujipanga kuelekea mbio za urais 2015, kiongozi huyo alisema hajazungumza na mtu kuhusiana na mambo hayo.
Sumaye alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na kunukuliwa kuwa zimetoka kwenye chanzo kilicho karibu naye, lakini akafafanua kuwa hawezi kupambana na Lowassa kwa sababu hana uhasama naye.
“Nikiamua kugombea urais sitagombea kwa sababu ya mtu fulani bali nitagombea kwa sababu ya nchi na wananchi wa Tanzania,” alisema.
Akifafanua kuhusu vitendo vya rushwa ndani ya CCM, alisema kuwa nchi nyingi hasa zenye demokrasia changa kama Tanzania zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi.
Sumaye alisema madaraka yatakuja tu kama wananchi wapiga kura wanaona wewe ndiye utayewafaa na wala wasirubuniwe kwa fedha au jambo lolote kwa kutumia vibaya nafasi ya umaskini wao.
“Hivi leo tunavyoongea hali ya rushwa wakati wa uchaguzi imekuwa mbaya zaidi. Katika uchaguzi wa kidemokrasia wapiga kura humchagua mwakilishi wanayemtaka kwa sababu ya uwezo wake yaani humchagua mwakilishi wao kwa ajili yao.
“Katika demokrasia iliyopondeka kwa rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha. Wapiga kura ni wapiga mihuri tu,” alisema.
Sumaye bila kutaja majina ya wahusika, alisema hali imetoka kwenye kuhonga ili achaguliwe katika eneo lake na badala yake kuna rushwa za kimtandao ambapo mtu hutoa fedha katika maeneo mbalimbali nchini ili watakaochaguliwa wawe wafuasi wake mbele ya safari atakapowahitaji.
“Uchaguzi huu umeghubikwa sana na matumizi makubwa ya fedha za rushwa. Suala la rushwa katika nchi yetu na katika CCM siyo mgeni lakini sasa tatizo hilo limeota mizizi na linazidi kuwa kubwa,” alisema.
Kuhusu kwenda CHADEMA

Sumaye alikanusha vikali akisema hajawahi kukutana na kiongozi yeyote wa CHADEMA wala chama chochote cha upinzani.
Lakini akabainisha kuwa hawapaswi kufikia kudai kuwa vyama vya upinzani au viongozi wake ni maadui wa CCM.
“Mimi ningekuwa nimekutana nao ningesema tu mbona hata hao wengine wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba huwa wanakutana nao? Alihoji.
Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM na kwamba alishawahi kusema kuwa hayuko kwa ajili ya cheo na wala kukosa ujumbe wa NEC na hasa kwa njia iliyotumika hakumnyimi usingizi wala hahuzuniki kugombea urais kwa tiketi ya CCM endapo ataamua kufanya hivyo.
Sumaye alisema kama ni matatizo, vyama vyote vina kasoro zake, hivyo haoni kama kuhama chama ni suluhu na kutamba kuwa kushindwa kwake kumempa nguvu zaidi na hivyo akiamua kugombea urais lazima apitie CCM.
Kuhusu TAKUKURU

Alipoulizwa kuhusu utendaji wa Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kama imetimiza wajibu wake kushughulikia tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi wilayani Hanang’, Sumaye alitafakari kidogo kisha akajibu kwa kutumia mfano.
“Hivi kama nyie wanahabari mmekuja hapa mkanisikiliza haya ninayowaeleza, halafu kesho watu wanasoma kwenye magazeti yenu hawakuti kitu au kwenye televisheni hawaoni, wanaweza kusema mmetimiza jukumu lenu? Alihoji Sumaye.
Kada huyo aliwaachia wanahabari watafsiri wenyewe kama kweli TAKUKURU inatimiza wajibu wake katika kushughulikia madai ya rushwa kwenye chaguzi.
“Napenda nitambue kuwa haya ninayoyasema si matamu masikioni mwa baadhi yetu lakini ni vema tukayasikiliza kwa makini na kuchukua hatua chanya ili yasilete madhara zaidi katika jamii na wala tusidiriki kuwanyamazisha wanaoyazungumzi