Saturday 27 September 2008

Kenya Prime minister Raila Odinga in Tanzania
Tanzania President Addresses the United Nations 2008 in his capacity as the chair of African Union
MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais Jakaya Kikwete, ametoa rai kwa nchi zilizoendelea kutoa misaada waliyoahidi katika nchi za Afrika. Akihutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mahitaji ya maendeleo ya Afrika mjini New York Marekani juzi, Rais Kikwete alisema anatumia nafasi hiyo kuelezea machungu ya nchi za Afrika kutokana na nchi zilizoendelea kushindwa kutimiza ahadi walizotoa katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo Afrika. “Naomba kutumia nafasi hii leo (juzi) kutoa changamoto kwa nchi zilizoendelea kutekeleza ahadi zao kwa kuwa ni jukumu lao la kihistoria kusaidia wahitaji Afrika, lakini huku tukikumbuka makubaliano ya Monterrey yaliyofanyika Machi 2002 na wakuu wa nchi duniani katika kusaidia kifedha nchi za Afrika,” alisema Rais Kikwete. Alisema ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inawakumbusha kwamba jambo linalozuia maendeleo ya Afrika ni kukosekana kwa mahitaji ya rasilimali kutokana na maendeleo kuhitaji kiasi kikubwa cha rasilimali, jambo linalosababisha nchi za Afrika kushindwa kujikwamua katika umasikini. Alisema serikali za Kiafrika zimekuwa zikichukua hatua katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa kutumia rasilimali ndogo zilizopo na zinazotokana na misaada ya jumuiya za kimataifa, lakini zimeshindwa kujikwamua na umasikini. “Kwa bahati mbaya, rasilimali hizo zimekuwa hazitoshi kusaidia Afrika kutoka kwenye wimbi la umasikini huku rasilimali nyingi ambazo nchi zilizoendelea zimekuwa zikiahidi wamekuwa hawatoi hivyo nchi za Kiafrika kuzidi kuwa masikini,” alisema Kikwete. Alisema nchi za Afrika zinashukuru kwa juhudi zinazochukuliwa katika utekelezaji wa makubaliano ya Monterrey yaliyofanywa na viongozi duniani, hata hivyo Afrika imekuwa na shaka kutokana na utofauti mkubwa wa kilichoahidiwa na kilichotolewa.Habari Zote kwa Hisani Ya Daily News..