Monday 8 October 2007

Umoja, amani na mshikamano London

Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho (Al-Baqara 126)
Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto
(Al-Baqara 201)
Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. (Al-Imran 8)
Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. (Al-Baqara 286)
Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika (Al-A'araf 23)
Ewe Mola Mlezi wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanao hukumu. (Al-A'araf 89)
Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. (Al-A'araf 126)
Wanachi wengi walijitokeza kwenda kufuturu katika msikiti wa ST ANN'S Tottenham, London. Picha zaidi ingia www.tanzaniaone.net